LOWASSA 'Aitikisa Tena Dar...KIBAMBA Yatapika People's.....Wamwambia 'ULIPO TUPO' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

LOWASSA 'Aitikisa Tena Dar...KIBAMBA Yatapika People's.....Wamwambia 'ULIPO TUPO'Mh. Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA, wakiwa jukwaani mbele ya umati wa watu

Wananchi wakionyesha alama ya mabadiliko inayotumiwa hivi sasa na UKAWA.

Mh. Lowassa, na Mwenyekitin wa CHADEMA, Mh. Mbowe, wakiwasili kwenye eneo la mkutano huko KibambaMgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda UKAWA, Mh. Edward Lowassa, leo tena amelitikisa jiji la Dar es Salaam, hususan maeneo ya Kibamba kulikofanyika mkutano wa kihistoria wa kampeni ambapo maefu ya wananchi walifurika wengine wakikaa juu ya mapaa ya nyumba za madarasa, wengine kwenye miti, kutokana na kukosa eneo zuri la kuweza kushuhudia "live" mkutanonukiendelea. Changamoto ya maeneo ya kufanyia mikutano ya kampeni ndiyo inayoonekana kuikumba UKAWA, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo. Pichani mfuasi wa UKAWA, akiwa amejichora rangi za bendera ya CHADEMA akiambatanisha maneno maarufu yanayotumiwa na wafuasi wa Mh. Lowassa kwa sasa, yaani "Ulipo tupo".


Mh. Lowassa, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kibamba, John Mnyika.(Picha zote na Othman Michuzi)


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.