Linex Akanusha Kutoa Wimbo "Because Of You" na Baraka Da Prince, Pata Ukweli Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Linex Akanusha Kutoa Wimbo "Because Of You" na Baraka Da Prince, Pata Ukweli Hapa

Msanii Linex anayefanya vizuri na ngoma ya Salima ft Diamond Platnumz amefunguka juu ya wimbo uliosambaa kwa kasi unaodaiwa kuwa amefanya na msanii Baraka Da Prince na kupewa jina la "Because of You" . "hio ngoma nlifanya nkiwa Kahama kwa ajili ya kumsaidia msanii flani ambae anaanza mziki ili apate mwongozo wa jinsi gani ataimba kwenye wimbo wake na nlikuwa na Baraka da Prince so nkaona na yeye aweke sauti yake ili huyu dogo aweze kuelewa atapitaje kwenye ngoma yake maana idea yake ilikuwa kama hii ila akawa hajui namna ya gani ya kupiga vocal nzuri, nashangaa yule producer kaunga zile vocal ametoa kama wimbo wangu na Baraka na kuupa jina "Because of You" , mimi sijatoa wimbo wowote na hio ngoma sio ndomana hata ukiskiliza ipo chini ya kiwango" alisema Linex.

Wimbo wenyewe Huu Hapo chini ; Sikilia hapo chini Linex Akiongea kuhusu Ishu ya Wimbo Huu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.