Jokate: Sijaona wa Kumwamini Kimapenzi...Kila Ninayemuamini, Anaishia Kuniliza ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jokate: Sijaona wa Kumwamini Kimapenzi...Kila Ninayemuamini, Anaishia Kuniliza !

LICHA ya kuzagaa kwa tetesi juu ya uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, mwanamitindo Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amesema kutokana na kuumizwa na mapenzi mara kwa mara, kwa sasa hajaona mwanaume wa kumuamini hivyo anaelekeza nguvu na akili zake kwenye kazi.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Jokate alisema ni ngumu kwa watu kuamini kuwa amekuwa akiumizwa na mapenzi mara kwa mara, kutokana na muonekano wa urembo alionao, lakini ukweli unabaki kuwa, anaumizwa na mapenzi na kwamba hana imani tena na wanaume.
“Kwa muonekano wangu wa juu, ni ngumu sana kuamini kuwa huwa naumizwa na mapenzi, hakika huwa naumia mno, kila ninayemuamini, anaishia kuniliza, sasa yatosha, simuamini mtu tena, sijamuona wa kumpa imani yangu kimapenzi, acha nielekeze nguvu na akili zangu kwenye kazi,” alisema Jokate.

Katikati ya wiki hii, Ali Kiba alinaswa Morogoro akiwa na mwanamke mwingine katika mazingira ambayo yaliashiria wana uhusiano wa karibu na kufanya watu waibue maswali.


By-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.