Jack Wolper na Mume wa Mtu Waangusha Pati ya Kufa Mtu..Licha ya Mke Kumtaka Wolper Aachane na Mumewe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jack Wolper na Mume wa Mtu Waangusha Pati ya Kufa Mtu..Licha ya Mke Kumtaka Wolper Aachane na Mumewe

Mume wa Mtu na Jack Wolper
KAMA mbwai na iwe mbwai! Licha ya mke kujitokeza na kumtaka aachane na mumewe, staa wa filamu Bongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’ bado amekuwa ni sikio la kufa baada ya hivi karibuni kuangusha pati ya nguvu ya kujipongeza kutokana na kuvishwa pete ya uchumba na mwanaume huyo ambaye ni raia wa Kongo.

Wolper na mchumba wake huyo mume wa mtu walifanya pati hiyo waliyosema ni kwa ajili ya chakula cha jioni kwa ajili ya kujipongeza kwa kuvalishwa pete ya uchumba iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Kempisk iliyopo Posta jijini Dar, waalikwa wakiwa ni marafiki zake wa karibu.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Wolper alisema kuwa wakati watu wakiendelea kuchonga kuhusiana na pete hiyo, kwake mambo yanazidi kumnyookea na wala yeye na mpenzi wake hawana habari.

Ninachojua ukweli wangu ninao na tayari mpenzi wangu kaniambia kila kitu na ndiyo maana sina habari na maneno wanayozungumza, wataona harusi tu na shela navaa kazi kwao wanaochonga kuhusu mimi maana kama huyo mke wanayemsema simfahamu,” alisema Wolper.
Katika gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda mke wa mchumba huyo wa Wolper alijitokeza na kumtaka aachane na mumewe lakini msanii huyo haoni wala hasikii.

chanzo: globalpublishers

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.