FRIENDS PUB YA SEGEREA NA CHECKPOINT CHANIKA BAA ZA WIKI TUSKER FANYA KWELI KIWANJANI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

FRIENDS PUB YA SEGEREA NA CHECKPOINT CHANIKA BAA ZA WIKI TUSKER FANYA KWELI KIWANJANI

Bet Sasa
Dj wa redio Efm, almaarufu Dj Con akitoa burudani ya muziki ndani ya baa ya Friends iliyopo Segerea jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani. Kampeni ambayo inaendelea pia kwa mikoa ya Arusha, Morogoro, Moshi, Mwanza na Mbeya.
Mkazi wa Chanika Kay Christopher akipokea zawadi yake ya fulana kutoka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (Kulia) wakati wa kuipongeza baa ya Check Point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwa mara ya pili kwenye Kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli kiwanjani. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash 
Mkazi wa Pugu (51) George Edward Koba akipokea zawadi yake ya fulana kutoka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (Kulia) wakati wa kuipongeza baa ya Check Point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwa mara ya pili kwenye Kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli kiwanjani. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash.
Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (katikati) akikabidhi zawadi ya fulana kwa mkazi wa Kigogo Fresh Mrs. Bakari Mnondwa (kulia) katika hafla ya kuipongeza baa ya Check point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. (Kushoto) ni Sada Mlore.

Septemba 29, 2015 Dar es Salaam, Kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani, imeendelea tena kuchukua sura nyingine wiki hii kwa wakazi wa jiji la Dar sambamba na mikoa ya Mwanza, Moshi, Mbeya, Arusha na Morogoro ambapo imeendelea kuziibua baa mbalimbali katika miji yote hiyo kama baa za wiki kupitia promosheni ya kila wiki inayodhaminiwa na bia ya Tusker kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti.
Kwa upande wa Dar es salaam, baa zilizotangazwa kwa wiki hii ni pamoja na Friends Pub ya Segerea na Check Point ya Chanika ambapo kama ilivyo ada siku ya Ijumaa Kampeni hii ilitikisa eneo la Segerea-Mwisho ambapo ndipo inapopatikana baa hiyo na kisha kuelekea Chanika katika baa ya Check Point siku ya jumamosi, hii ikiwa ni mara ya pili kwa baa hiyo kutembelewa na promosheni hii kutokana na wingi wa wateja wa bia ya Tusker jambo ambalo liliwavutia mameneja wa bia hiyo.
Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inaendelea kujizolea sifa katika umahiri wake wa burudani, muziki, washereheshaji na zawadi kem kem kwa wateja wake huku ikirushwa  moja kwa moja kupitia redio E-fm kuanzia saa mbili jioni hadi saa sita usiku. Akizungumza na Mshereshaji wa promosheni hiyo baada ya kupewa nafasi, mkazi wa Kinyerezi Zack Ngaweleja shabiki aliyefika eneo la tukio katika baa ya Friends-Segerea alisema …“Nimekua mtumiaji mzuri wa bia hii ya Tusker kwa miaka takriban mitano sasa na kikubwa kinachonivutia ni ladha yake. Awali nimekua nikisikia tu matangazo ya promosheni hii kupitia redio Efm na nikaona ni vema wiki hii nimeweze kujimuika na wapenzi wengine wa bia hii katika kuipongeza baa yetu hii ya karibu”.
Kampeni ya Tusker Fanya Kweli Kiwanjani imemaliza takribani wiki saba sasa ikizunguka baa kwa baa jijini Dar pamoja na mikoani na hadi sasa imezifikia baa zaidi ya 400 ambapo haya ni mafanikio makubwa kwa upande wa bia hiyo kutokana na  kuvuka nusu ya matarajio ikiwa kampeni hiyo bado inaendelea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika baa ya Friends Segerea, Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi Nandi Mwiyombella alitoa pongezi na shukrani kwa mashabiki kufurika wakati wa promosheni hiyo kusherekea na bia waipendayo ya Tusker huku akisitiza kuwa Kampeni bado inaendelea na lengo likiwa ni kuzifikia baa 1000.  
“Tunaendelea kuguswa katika kuwaonesha wateja wetu kwamba tunawathamini na kuwashukuru kwa kuwa pamoja nasi katika safari hii na waendelee kusherekea na kuburudika na Tusker”. Aliongezea kwamba Chapa ya Tusker imejitosheleza katika kuhakikisha kwamba kampeni inakuwa kubwa na yenye ubora wa kipekee ndani na nje jiji la Dar es salaam.
Promosheni hii ilienda sambamba na ile iliyofanyika jijini Mwanza katika baa ya Siwa na Shooters siku ya Ijumaa na Jumamosi. Baa hizi zilifanikiwa kujinyakulia ushindi wa kufanyiwa promosheni hiyo baada ya kuzipiku baa nyingine sita zilizokuwa zikishindanishwa kwa wiki iliyopita.
Ili kufuatilia kwa ukaribu kampeni hii, wakazi wa Dar wanaweza kusikiliza kipindi cha Ubaoni cha E-fm ambacho kinaruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tisa mchana mpaka saa moja usiku na kufuatilia promosheni za Fanyakweli Kiwanjani zikirushwa hewani moja kwa moja ni siku za Ijumaa na Jumamosi kuanzia saa mbili usiku. Mikoani Mbeya ni Bomba fm katika kipindi cha “Afri carnival” kinachoruka kuanzia saa moja hadi mbili na nusu jioni, Arusha ni Radio-5 kwenye kipindi cha “Drive time antenna show” kinacho anza saa kumi na nusu hadi kumi na moja jioni, Morogoro ni Planet Fm kwenye kipindi cha “Planet base show” kinachoruka saa kumi na moja hadi saa mbili usiku na Kilimanjaro ni Kili Fm katika kipindi cha “kili drive show” kinacho anza saa kumi na moja hadi kumi na nusu jioni kwa maelezo zaidi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.