Diamond atoa sababu za kutomwonesha Tiffah sura yake mpaka siku 40. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond atoa sababu za kutomwonesha Tiffah sura yake mpaka siku 40.

Diamond Platnumz ametoa sababu ya kwanini yeye na Zari wameamua kutomwonesha sura mtoto wao Tiffah mpaka siku arobaini (40) zipite.
mondi na tiffah
Mpaka sasa picha zote zaTiffah ambazo Diamond na Zari wanaziweka kwenye mitandao ya kijamii hazimuoneshi sura yake.
tiffah
Akizungumza kupitia kipindi cha Uhondo cha E-FM kinachoongozwa na Dina Marios, Diamond amesema kuwa yeye na Zari walikuwa wanafanya mazungumzo na baadhi ya makampuni yatakayo endorse kupitia picha ya Tiffah itakayomuonesha sura kwa mara ya kwanza.
“Tulikuwa tunasubiri kuna baadhi ya kampuni ambazo kwa mara ya kwanza sura yake ikiwa inaonekana tunataka zi endorse,” alisema Diamond. “Sababu ile picha itasambaa kwa hiyo itakuwa inatangazwa na yale makampuni, tulikuwa tunamalizana nao na tumepanga siku 40 ndo mara ya kwanza.”
Kutokana na mipango hiyo Dimaond amesema kuwa wamejitahidi sana kutoruhusu mtu yeyote kumpiga mtoto picha katika kipindi hiki kabla siku 40 hazijafika, ili isije kusambaa na kuharibu mchongo mzima. Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.