DAVIDO ATANGAZA UJIO WA COLABO YAKE NA JOH MAKINI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

DAVIDO ATANGAZA UJIO WA COLABO YAKE NA JOH MAKINI

Bet Sasa
Ndicho kilichotokea usiku wa Sept 18 pale staa wa Nigeria, Davido alipotweet kuwa kuna collabo yake na Joh Makini inakuja.
Hakuna surprise nzuri kama ile ambayo hukuwahi kuona hata dalili, na kwenye muziki hasa kwa msanii wa Bongo hakuna kitu kizuri kama msanii mkubwa wa nje kuanza kutease ujio wa kazi yenu hata kabla yako.
 
Bado haijajulikana kama ni wimbo wa Davido kamshirikisha Joh Makini au Joh kamshirikisha Davido au ni wa wote.
Hii ni hatua nyingine kubwa ya safari ya Joh Makini kwenda kimataifa, baada ya kufanya collabo na AKA na kuwa kwenye matayarisho ya kufanya collabo nyingine na rapper KO wa Afrika Kusini, mashabiki wa rapper huyo wa Weusi watarajie collabo hiyo ya Davido na Mwamba wa Kaskazini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.