B.O.B Naye Kudondoka Afrika Mashariki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

B.O.B Naye Kudondoka Afrika Mashariki

Msanii wa kimataifa kutoka Marekani, Bobby Ray Simmons, maarufu zaidi kama B.O.B anatarajiwa kutua Afrika Mashariki mwishoni mwa mwaka huu, ambapo atatumbuiza huko nchini Kenya katika tamasha kubwa litakalofanyika Desemba 12.
Msanii wa muziki kutoka Marekani B.O.B
Ujio wa staa huyo mwenye rekodi ya kushinda tuzo za kimataifa, unakuja baada ya mastaa wakubwa kama Akon, 2 Chainz, na Neyo kati ya wengine, kufika nchini humo mwaka huu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za burudani, ikiwepo kutumbuiza.
Hii itakuwa ni nafasi nzuri ya wasanii mbalimbali wa muziki na wadau kuweza kufanya kazi na kubadilishana mawazo katika kukuza sekta ya muziki kimataifa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.