Afande Sele "Wanamuziki Wengi Bado Wanaishi Lakini Muziki Umekufa" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Afande Sele "Wanamuziki Wengi Bado Wanaishi Lakini Muziki Umekufa"

Rapper mkongwe nchini, Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele, amesema wanamuziki wengi wanaweza kuwa hai lakini muziki wao umekufa.
Afande-Sele-nzuri_full
Afande ameiambia Bongo5 kuwa muziki umeingiliwa na wasanii wanaofanya biashara ya muziki bila kuwa na wito na kazi hiyo.
“Wanamuziki wengi wa zamani wa kizazi kipya hata wale wa zamani akina Mbaraka, Majani wametangulia mbele ya haki na wengine wapo pamoja na wanamuziki wa kizazi kipya ambao hawajafariki dunia, lakini kimuziki ni kama hawapo lakini nyimbo zao bado zinaishi. Ila wanamuziki wa sasa hivi unakuta ndio wapo na vyombo vya habari vinawatangaza na wapo kwenye peak za juu lakini bahati mbaya nyimbo zao haziishi hata kidogo,” amesema.
“Wanamuziki wengi bado wanaishi lakini muziki wao umeshakufa. Lakini yote haya ni kwa sababu ya mtazamo wa kibiashara/ Leo hii muziki umekuwa sio wito tena, kila mtu akiwa na mtaji wake anaingia na anafanya poa. Kwahiyo sasa waandishi wa habari, wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wadau wa muziki waangalie hili vinginevyo hatusaidii kukua kwa muziki.”

-Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.