WALIMU TANZANIA NZIMA WAAPA KUMPIGIA KURA LOWASSA KAMA ATAKUBALI KUTEKELEZA HAYA, SOMA HAPA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

WALIMU TANZANIA NZIMA WAAPA KUMPIGIA KURA LOWASSA KAMA ATAKUBALI KUTEKELEZA HAYA, SOMA HAPA


Mimi Edward Lowasa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naapa kuwa endapo nitachaguliwa kuwa rais nitatekeleza ahadi iliyoshindikana kwa miaka mingi ya kuboresha elimu ya mtanzania kwa kufanya yafuatayo:
Nitahakikisha walimu wanalipwa Stahiki zao zote kwa wakati.
Nitahakikisha madeni yote ya walimu yanalipwa ndani ya mwaka mmoja.
Nitahakikisha walimu wanapata teaching allowance & house allowance.
Nitahakikisha Mishahara ya walimu inalipwa kulingana na viwango vya elimu ikilinganishwa na kada nyingine kama afya.
Nitaweka posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu.
Nitahakikisha kila mwanafunzi anakalia dawati/kiti na ana meza.
Kila shule itapata computers kwaajili ya kufundishia wanafunzi na somo la computer litakuwa la lazima. Nitajenga maabara ya computer kila shule ya sekondari.
Nitaondoa michango yote mashuleni ikiwemo michango ya ulinzi, taaluma, ujenzi//ukarabati nk. Serikali . Itasimamia sehemu hiyo kwa ustadi mkubwa kuhakikisha walinzi wanalipwa na serikali, shule zinapata walimu wa kutosha, ujenzi/ukarabati unasimamiwa na serikali na unafanyika kwa wakati.
kama hayo niliyoyataja hayatatekelezwa ndani ya miaka 2 ya uongozi wangu, nitajiuzuru ili nishitakiwe kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusema uongo na kuwalaghai watanzania.


............................. ..
EDWARD N. LOWASA
............................
Tarehe

Kiapo hiki kimesainiwa Mbele ya mwanasheria mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

.............................. .....
TUNDU A. LISU
MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA


-RT Blog

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.