Upweke wamchosha Shamsa Ford sasa atamani ndoa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Upweke wamchosha Shamsa Ford sasa atamani ndoa

Bet Sasa
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kuweka wazi hisia zake za kutaka kuolewa na kusema kwa sasa yupo tayari kuvunja minyororo ya ubachela na kuingia katika maisha ya ndoa kama mke wa mtu.
Shamsha ameweka wazi hisia zake hizo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema kuwa yupo tayari kuolewa sababu amechoshwa na maisha ya kuwa peke yake ingawa anadai kuwa anatamani mtu ambaye atamuoa awe mtu asiye kuwa na umaarufu wowote kwani hataki maisha yao yatawaliwe na skendo.
"Sijui hizi hisia zimetoka wapi...kwa sasa natamani kuolewa na nipo tayari kuolewa ila na mtu ambae si maarufu. Maisha ya usingle nimeshayachoka," Ukurasa wa Shamsa Ford wa mtandao wake wa Instagram ulisomeka maneno hayo ya kuonyesha amechoshwa na upweke.
Hata hivyo siku za nyuma kulikuwa na tetesi kuwa Shamsa Ford anatoka kimapenzi na msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego ambapo wenyewe hawajawahi kukiri wazi kuwa ni wapenzi ingawa kuna picha mbalimbali zilikuwa zikiwaonyesha kama wapenzi kutokana na namna ambavyo picha hizo walikuwa wakizitumia katika mitandao yao ya kijamii jambo ambalo kwa mashabiki lilitoa tafsiri ya haraka kuwa watu hao wana mahusiano ya mapenzi.
-eatv

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.