Ujue wasifu wa mgombea urais Chadema, Edward Lowassa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ujue wasifu wa mgombea urais Chadema, Edward Lowassa

lowassa
Edward Ngoyai Lowassa akitoa hotuba yake leo.
Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa tarehe 26 August 1953, katika kijiji cha Ngarash wilayani Monduli mkoa wa Arusha, akiwa ni mtoto wa 4 kati ya watoto 23 wa mzee Ngoyai Lowassa.
Edward Lowassa amemuoa Regina Lowassa na kujaliwa kupata watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike.
lowassa 2
Lowassa akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.
ELIMU:
1961 – 1967: shule ya msingi Monduli
1968-1971: shule ya sekondari Arusha
1972 – 1973: St. Marry’s High School (Milambo High School) Tabora.
1983 – 1984: Chuo Kikuu cha BATH Uingereza M.Sc (Development Studies).
lowassa 3
Mhe. Edward Lowassa mgombea urais akiwa na mgombea mwenza Juma Haji Duni.
UZOEFU KAZINI:
1977-1978: Katibu Msaidizi ccm mkoa wa Shinyanga
1979-1982: Katibu Mtendaji ccm mkoa wa Arusha.
1983-1985 – Katibu mkuu msaidizi ccm Mkoa wa Kilimanjaro.
1985-1995 – Mbunge wa umoja Vijana wa ccm.
1989-1990 – Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha mikutano cha kimataifa (AICC) Arusha.
1990-1993 – Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais anayeshughulikia sera, Uratibu Bunge, Maafa namasuala ya mahakama.
1993-1995 – Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya miji.
1995-2005 – Mbunge wa Monduli (ccm)
lowasa 5 Lowassa akiwa na mgombea mweza Juma Haji Duni (kushoto) pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika picha ya pamoja leo.
1995 – 2000 – Waziri nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira, Muungano nakuondoa umasikini.
2000 -2005 – Waziri wa maji na maendeleo ya mifugo.
Desemba 2005 Februari 2008 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
1985 – 2005 – Mbunge wa Monduli (ccm)
2010 – 2011 – Mwenyekiti Kamati ya bunge ya ulinzi na usalama na mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa .
2011 – 2015 – Mwenyekiti kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
28/07/2015 – Kujitoa CCM na kujiunga na CHADEMA
Mhe. Edward Lowassa ni shabiki wa michezo na alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.