SIASA: Kauli Ya Lowasa Yaiumiza Kichwa CCM. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SIASA: Kauli Ya Lowasa Yaiumiza Kichwa CCM.


Akizungumza na wajumbe kwenye Mkutano Mkuu jijini Dar es Salaam Lowassa amesema, hakuna sababu ya kutoa lugha za matusi huku akiwasihi kuimarishwa kwa amani wakati wa uchaguzi huo. 

“Muungano huu una nguvu kubwa ya kwenda kuchukua dola saa 2:30 asubuhi, na tutachukua dola asubuhi,” amesema Lowassa na kuongeza; “hatuko tayari kuibiwa kura na hatutafanya fujo lakini wasiibe kura zetu.”


Amesema kuwa, katika maisha yake hana msamiati wa kushindwa isipokuwa ana msamiati wa kushinda huku akiwataka wana Chadema na UKAWA kuwa wamoja katika kukidondosha Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.