SBL YAPELEKA UZINDUZI WA TUZO YA UBORA WA THAMANI KWA WAKAZI WA MWANZA NA MOSHI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SBL YAPELEKA UZINDUZI WA TUZO YA UBORA WA THAMANI KWA WAKAZI WA MWANZA NA MOSHI

Meneja mauzo  kanda ya ziwa,  Samuel Kisyombe (kushoto) na (Kulia) ni Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji  wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Denis Tairo pamoja na mabalozi wa bia ya Serengeti Premium Lager wakizindua kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection kwa wateja wa kanda ya ziwa jijini Mwanza ambapo bia hiyo toka SBL imetuzwa medali tatu za dhahabu kutoka kwenye viwanda vyake vyote vitatu; cha Dar es salaam, Mwanza na Moshi kwa mwaka 2015. Sherehe ya kuzindua kampeni ya ‘Tunaijua Bia na Serengeti Premium Lager Ndio yenyewe’ ilifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza.
Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji  wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Denis Tairo akizungumza na wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager wakati wa uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection kwa wakazi wa kanda ya ziwa jijini Mwanza ambapo bia ya Serengeti Premium Lager ya SBL imetuzwa medali tatu za dhahabu kutoka kwenye viwanda vyake vyote vitatu; cha Dar es salaam, Mwanza na Moshi kwa mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza.
Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji  wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Denis Tairo akikabidhi kiasi cha Tsh 50,000 fedha taslim kwa mkazi wa Kona ya Bwiru,jijini Mwanza Bw. Godfrey Urio aliyeibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta” wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu kutokana na ubora wake.Hafla hiyo ambayo ilikua mahususi kwa wakazi wa kanda ya ziwa, ilifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza. Shindano hilo litafanyika Tanzania nzima na kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa kitaifa. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.
Wakazi wa Majengo mjini Moshi wakiburudika kushangilia Tuzo ya Dhahabu ya Monde waliyoipata kwa Bia ya Serengeti Premium Lager mwaka 2015 kutambua ubora wa kiwango cha juu wa iliyopata Bia ya Serengeti Premium Lager ambayo iliambatana na mashindano ya kutambua bia ya Serengeti Premium Lager mwishoni mwa wiki katika Baa ya Oriental. 
Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Brewieries Limited wakiwa na Mabalozi wa kinywaji hicho wakati wa  kutambulisha Tuzo ya Dhahabu ya Monde inayotambulika kimataifa baada ya bia ya Serengeti Premium Lager kukidhi viwango vya juu vya ubora katika hafla iliyofanyika katika Baa ya Oriental , Majengo mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.