PENNY AGOMEA AROBAINI YA TIFFAH - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

PENNY AGOMEA AROBAINI YA TIFFAH


Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kusema kuwa hata akialikwa kwenye sherehe ya arobaini ya mtoto wa ‘x’ wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Tiffah hawezi kwenda pamoja na ushkaji wao kwa sababu mpenzi wake wa sasa hawezi kumruhusu. 
Akizungumza na Ijumaa Penny alisema kuwa hawezi kwenda kwenye sherehe hiyo kwa sababu Diamond ni mtu ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi huko nyuma hivyo kwenda kwenye sherehe hiyo ni moja ya kumkwaza mpenzi wake wa sasa.
“Sina ubaya na Nasibu lakini siwezi kukanyaga kwenye sherehe ya mtoto wake kwa sababu siwezi kueleweka kwa baby wangu, kama mapenzi tulimaliza kitambo tutakutana tu kwa mambo mengine lakini siyo mimi kujibeba na kwenda kwake,” alisema Penny
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.