Nicki Minaj ajitangaza kuwa mjamzito baada ya kumuita Meek Mill 'Baby Father' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nicki Minaj ajitangaza kuwa mjamzito baada ya kumuita Meek Mill 'Baby Father'

RAPA wa kike aliyejizolea umaarufu kutoka lebo ya Cash Money, Nicki Minaj hivi karibuni ametangaza kuwa ni mjamzito.
Nicki (32) aliweka wazi alipokuwa jukwaani katika tamasha kubwa lililojumuisha ziara yake ijulikanayo kama Pinkprint huko Pennsylvania ambapo alipanda na mchumba wake, Meek Mill na kusema;
“Piga kelele kwa baba wa mtoto wangu!”

Baada ya shoo hiyo, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nicki aliweka kipande cha video hiyo akizungumza maneno hayohayo sambamba na kuambatanisha kikatuni (emoji) ya kulia.

Kwa kipindi kirefu Nicki amekuwa na uhusiano na Meek Mill ambapo hivi karibuni uhusiano wao ulidaiwa kuteterereka kwa kile kilichoelezwa ni kutupiana matusi kwa Meek na Drake kwenye nyimbo zao na mitandao ya kijamii.


-tubongetz

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.