Ni kweli Mourinho alikataa kupeana mikono na Wenger ? Jibu lipo hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ni kweli Mourinho alikataa kupeana mikono na Wenger ? Jibu lipo hapa

Bet Sasa
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho August 5 amerudi tena kwenye headlines baada ya kulizungumzia tukio la yeye kutopeana mkono na kocha wa Arsenal Arsene Wenger katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliopigwa August 2 katika Uwanja waWembley London.
Defender-Filipe-Luis-quitting
Mourinho huwa na desturi ya kutoa kauli mbalimbali ambazo wengine utafsiri kama kuwavunjia heshima lakini wengine huchukulia kama sehemu ya mchezo, sasa August 5 katika mahojiano Mourinho amejibu kuwa hakukataa kupeana mikono na Wenger kwani ni heshima kwa klabu yake hawezi kukataa kupeana mikono na kocha mwenzie.
Real-Madrids-Jose-Mourinh-007
“Mtazamo wangu ni huu hapa ni kama kitu kimoja kipo mtaani na kingine kipo uwanjani, Kama kocha uwanjani siwezi kukataa kupeana mkono na mpinzani kwa heshima ya klabu yangu na kwa heshima ya mchezo wa mpira wa miguu kamwe nisingeweza kukataa kupeana mikono na kocha Uwanjani”>>>Mourinho
1412517546264_wps_25_Chelsea_V_Arsenal_5_10_20
Kocha huyo huwa na kauli ambazo kocha wa upande wa pili ni lazima uwe na uvumilivu wa kusikia chochote kutoka kwa Mourinho kama timu zenu zinakaribia kukutana ni lazima atumie mbinu ya kutaka kukutoa mchezoni.
Nimekuwekea video ya kilichotokea katika mchezo wa August 2

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.