Mwigizaji Kajala Naye Ajitokeza na Kumtaja Mgombea wa Urais Anaye Mpigia Debe..Huyu Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwigizaji Kajala Naye Ajitokeza na Kumtaja Mgombea wa Urais Anaye Mpigia Debe..Huyu Hapa

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka kuwa kutoonekana kwake kwenye ushabiki wa vyama na wagombea kama wasanii wengine si kwamba hana ushabiki lakini moyoni mwake yupo Team ya Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kajala aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa pamoja na mbwembwe za watu kujiweka wazi kuhusu chama na wagombea wanaowakubali, yeye mambo yake ni kimyakimya kama alivyo mgombea wake wa urais kupitia chama hicho.
“Nimekuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu hata mgombea wangu wa urais, Magufuli ni mtu wa kimyakimya ila mtendaji mzuri, ndiye anastahili kura yangu,” alisema Kajala.

Source:Global Publishers

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.