Mwigizaji Elizabeth Michael "Lulu" Azama Katika Maombi! Ipo hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwigizaji Elizabeth Michael "Lulu" Azama Katika Maombi! Ipo hapa

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa sasa yupo ‘bize’ kwenye maombi kwa Mungu, kutokana na kile alichokiita, kutumia muda mwingi kuwa katika ibada za kumcha Mungu.
ElizabethMichaellulu.jpg
Jumapili iliyopita, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila walinaswa na mwandishi wetu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa Albamu ya Tunapendwa na Mungu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Boniface Mwaitege.
Hata hivyo, mwandishi wetu alipomuuliza Lulu kulikoni kuzama kwenye maombi, alijibu kwa kifupi kuwa katika maisha ya duniani hakuna jipya, hivyo yeye na familia yake wameona ni heri kumkabidhi Mungu maisha yao, ikiwa ni njia sahihi ya kutafuta faraja ya kweli na uzima wa milele.
Hata hivyo, Lulu hakueleza kwa undani kile alichokiita kuchoka na sarakasi za kidunia huku muda wote wakati anazungumza na mwandishi wetu akilitaja jina la Yesu.
“Sikiliza, sina muda wa kuzungumza na wewe, kama unavyotuona hapa na mama yangu (akimgusa begani), tumeamua kujiweka miguuni mwa Mungu, hapa duniani hakuna jipya tena, natumia muda wangu mwingi kumtumikia Mungu, kila mahali palipo na mkusanyiko wa ibada kama hivi, hakika sikosi, moyo wangu unafurahia kumwabudu Mungu kuliko kufanya mambo ya kijinga.
“Kwa hiyo, mimi na mama yangu kwa sasa tumejiweka mbali na ulimwengu, kwanza niache niendelee na maombi,” alisema Lulu huku akifumba macho kwa hisia kali.
Kwa upande wake mama Lulu aligoma kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo.

-gpl

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.