MANENO YA MOURINHO BAADA YA KUKUBALI KIPIGO TOKA KWA CRYSTAL PALACE AKIWA NYUMBANI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MANENO YA MOURINHO BAADA YA KUKUBALI KIPIGO TOKA KWA CRYSTAL PALACE AKIWA NYUMBANI

Chelsea Vs Crystal Palace
Jose Mourinho amesema timu yake ilistahili ushindi kwenye mechi ya leo dhidi ya Crystal Palace ambayo wameshindwa kwa 2-1 wakiwa nyumbani Stamford Bridge.
Chelsea Vs Crystal Palace
Bao la Joel Ward katika dakika ya 81 ndio liliizamisha Chelsea ambayo muda kidogo kabla ilikua imesawazisha bao la kwanza kupitia Radamel Falcao.
Chelsea Vs Crystal Palace
Kwenye mechi hii, Chelsea wamepata mashuti 26 huku tisa pekee ndio yakilenga golini ambapo Mourinho anasema sare ndiyo ilikua wanaistahili kwa mchezo wa leo.

"Hongera kwao Palace. Ni matokeo mazuri kwao na perfomance nzuri" aliiambia BBC SPORT.

"Hatukustahili kupoteza. Lakini Palace wametupa mchezo mgumu. Matokeo yalitakiwa iwe sare ,ambayo isingekua mbaya kwetu. Tumepambana vya kutosha."
Chelsea Vs Crystal Palace
Baada ya kupoteza mechi ya leo, sasa Chelsea wako nyuma ya point nane kwa Man City ambao wameendelea kujihakikishia ushindi wao kwa asilimia 100 baada ya kuwapiga Watford 2-0.

VIKOSI:Chelsea: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Pedro, Willian, Hazard, Costa
Akiba: Begovic, Baba, Falcao, Mikel, Remy, Loftus-Cheek, Kenedy.

Crystal Palace: Alex McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Cabaye, McArthur, Zaha, Puncheon, Sako, Wickham
Akiba: Mariappa, Bolasie, Hennessey, Lee, Gayle, Mutch, Ledley.
REFA: Craig Pawson 
MATOKEO KWA UJUMLA MECHI ZA JUMAMOSI TAREHE 29/8/2015

Newcastle 0 Vs Arsenal 1
Aston Villa 2 Vs Sunderland 2 
Bournemouth 1 Vs Leicester 1 
Chelsea 1 Vs Crystal Palace 2 
Liverpool 0 Vs West Ham 3 
Man City 2 Vs Watford 0 
Stoke 0 Vs West Brom 1 
Tottenham 0 Vs Everton 0

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.