Lulu Apata Pigo, Afiwa na Bibi Yake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Apata Pigo, Afiwa na Bibi Yake

Staa mwenye umri mdogo anayekimbiza katika filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata pigo baada ya kufiwa na bibi yake mzaa mama, Leonadina Mboneko, aliyefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Masana, iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Amani mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila alisema mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu jambo lililomlazimu kumtoa nyumbani kwake Bukoba na kumleta jijini kwa ajili ya kupata matibabu.
“Nimehangaika naye kwa muda mrefu ili kurejesha afya yake, lakini hali ilikuwa ngumu hadi juzi Mwenyezi Mungu alipomchukua. Tumepata pigo kubwa sana hasa mwanangu Lulu kwa sababu alikuwa ndiye kipenzi chake,” alisema mama huyo.
Muigizaji huyo aliyecheza Filamu ya Foolish Age hakuweza kupatikana kuzungumzia msiba wa kipenzi chake huyo, lakini nyumbani kwa mama yake, mipango ya kusafirisha mwili huo kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya mazishi ilikuwa ikifanyika.
Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Lulu aliweka picha hiyo hapo juu na kuandika  
“Kama Binadamu Kuna Muda Unaweza kujikuta unamkufuru Mungu...lakini Kwa Upande mwingine Naamini Mungu ameniamini Nayaweza yote haya Na ndo Maana Ameyaruhusu yapite Kwangu....!
Jina Lako Lihimidiwe  Nenda Kwa Amani Bibi Yangu...Pumzika Kwa Amani Pacha Wangu
May Ur Soul Rest In Peace Twinnie”
RIP bibi
Chanzo: GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.