Licha ya Kupata Bwana Mpya; Johari: Siachani na Ray ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Licha ya Kupata Bwana Mpya; Johari: Siachani na Ray !

SIKU chache baada ya kupenyezwa kwa madai ya kupata bwana mpya, staa wa filamu Bongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kamwe hafikirii wala hana mpango wa kuachana na msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ katika masuala ya kazi.
Akianika mwanya’ na Risasi Jumamosi hivi karibuni ndani ya ofisi zake, Sinza-Mori jijini Dar, Johari alisema hawezi kuruhusu mapenzi yatawale maisha yake na kusahau kazi.
“Siondoki RJ, kama kuna mtu anatarajia nitoke hapa eti kisa mambo ya mapenzi, anajidanganya kabisa, sifikirii kuachana na Ray kikazi, ni mtu muhimu sana, mapenzi hayawezi kutawala maisha yangu, yeye atabaki na mpenzi wake na mimi nitaendelea na mpenzi wangu,” alisema Johari.
Ray kwa sasa ameshaonesha upande na kukiri kukolea kwenye penzi la mwigizaji  Chuchu Hans na tayari ameshajipambanua kuwa wana mipango endelevu maishani mwao.
Chanzo: GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.