Kolabo ya Alikiba na Fally Ipupa inakuja muda sio mrefu, Kiba Afunguka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kolabo ya Alikiba na Fally Ipupa inakuja muda sio mrefu, Kiba Afunguka

Bet Sasa

Alikiba amesema tayari ameshafanya kolabo na msanii wa Congo DRC, Fally Ipupa na kwamba ukifika wakati itatoka.

Alikiba ambaye yupo kwenye mikakati ya kufanya kolabo na Davido, ameiambia Clouds TV kuwa ikifika wakati ataiachia kolabo hiyo ambayo amedai ipo tayari.
“Mwana ilikuwa ni nyimbo ambayo nifanye na Fally Ipupa, beat imetengenezwa na Man Walter. Lakini kitu ambacho kilikwenda kutokea wakati nakwenda studio kufanya nyimbo nyingine kabisa, nikakuta Man Walter ameniandalia beat, ‘ile nyimbo yako unataka kufanya na Fally Ipupa hii hapa.’ Akaweka beat nikaanza ku-flow pale, nikaimbaimba nikapata melody. Kesho yake nikarudi nikafanya demo, kufanya demo nikarudi nyumbani nikakaa kama wiki, baada ya wiki moja nikaenda nikaimaliza yote,” alisema Kiba.
“Lakini sasa tukakaa na Man Walter nikasema Fally Ipupa anaimbaje hapa? Akasema kwa kweli umeperfome vizuri sana, mimi naona ume-perfome vizuri sana. Tukapanga tufanye nyimbo nyingine. Basi akasema poa lakini Mwana ilikuwa Fally Ipupa aimbe. Kolabo na Fally Ipupa ipo, lakini kama ilivyo kawaida yangu napendaga kuwa-surprise watu kwa sababu watu wanakuwa hawajui Ali anafanya kitu gani muda wowote. Lakini ngoma ya Fally na mimi ipo na siwezi sema ni nyimbo gani lakini nyimbo ni nzuri sana na imesharekodiwa,” alisema Alikiba.
Pia Alikiba amesema kolabo yake na Davido ipo kwenye hatua nzuri na muda ukifika mashabiki wa muziki wake watajua lini itatoka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.