KISUMA NA SAFARI RESORT BAA ZA WIKI KWENYE SHINDANO LA TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

KISUMA NA SAFARI RESORT BAA ZA WIKI KWENYE SHINDANO LA TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI

Dj wa E-fm anayetambulika kwa jina la Dj Skit, akiporomosha burudani ya muziki ndani ya baa ya Safari resort ya Kimara jijini Dar wakati wa hafla ya kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki wa kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani. Lengo la kampenii likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli wanapotoa huduma kwa wateja.
Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo Bw. Victor Mhindi akikabidhi zawadi ya polo shirt kwa Papaa Mazengo mkazi wa Kimara wakati wa promosheni ya Fanyakweli kiwanjani katika baa ya Safari resort. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa shindano hilo baada ya kupigiwa kura na wateja wa baa hiyo. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner G. Habash.

Meneja wa baa ya Safari resort Kimara Bw. Robert Herman akielezea furaha yake baada ya baa yake kutembelewa na promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani huku akifafanua kuwa kiwanja hicho kilichopo Kimara jijini Dar es salaam ni mahali tulivu sana kwa wateja. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker.
Bi Grace Mweleke (Katikati) akipokea zawadi ya fulana kutoka kwa Meneja wa baa ya Safari resort iliyopo Kimara jijini Dar Bw. Robert Herman wakati wa promosheni ya Fanyakweli kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker  ilipofunga kambi kiwanjani hapo kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo (Kushoto) ni mshereheshaji wa shindano hilo Gadner G. Habash.
Mkazi wa Temeke Bi. Anna Sylvester (Katikati) akipokea zawadi ya polo shirt baada ya kushiriki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani alipojumuika na marafiki zake kuipongeza baa ya wiki ya Kisuma iliyopo Tandika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanya kweli kiwanjani wiki hii.(Wa kwanza kulia) ni rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Tatu Mohammed, (Wa pili kulia) ni Mshereheshaji wa shughuli hiyo Gadner G. Habash sambamba na wasimamizi wa bia hiyo toka SBL.
Mkazi wa Mwembeyanga Bw. Frank Kabisi (katikati) akifurahia zawadi yake ya mfuko na Tisheti alizopewa wakati wa wa hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma iliyopo Mwembeyanga Tandika mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker toka kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani na Tusker Gadner Habbash na (kulia) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi.
Bi. Catherine Bonventure (Katikati) Mkazi wa Temeke akipokea zawadi ya kalamu pamoja na bia za bure kutoka kwa mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash (Kulia) kwenye kiwanja cha Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo ya Tandika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo lake likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli kwa kwa wateja wakati wa utoaji huduma. (Kushoto) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.