BREAKING NEWS: WANACHAMA WA CUF WAVAMIA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA CUF LEO - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

BREAKING NEWS: WANACHAMA WA CUF WAVAMIA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA CUF LEO

Bet Sasa
WANACHAMA wa Chama cha Wananchi (CUF) wamevamia makao makuu ya chama hicho leo asubuhi na kusababisha kikao cha mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba na wanahabari kuhairishwa.


Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba

Mkutano wa mwenyekiti huyo ulikuwa ufanyike leo saa nne asubuhi makao makuu ya Cuf yaliyopo Buguruni, Dar es Salaam lakini hadi saa tano, mwenyekiti alikuwa kwenye kikao cha ndani na “wazee wa chama” waliokuwa wanataka ufafanuzi kwa baadhi ya mambo.
“Wazee wanataka ufafanuzi kwa baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na taarifa zilizoenea kuwa amejiuzulu,” amesema Magdalene Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara amewaamabia wanahabari.
Hata hivyo, wananchama waliokuwa nje wakati mwenyekiti Lipumba akiendelea na kikao cha ndani cha chama hicho walionyesha kushtushwa na taarifa zilizochapishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuwa Profesa Lipumba ameachana na siasa za chama hicho.
Wasiwasi huo uliongezeka jana mara baada ya mtaalamu huyo wa uchumi kutoonekana wakati wa kumtangaza Edward Lowassa kuwania urais kupitia Chadema, moja ya chama kinachounda Ukawa huku Juma Duni Haji akipitishwa kama mgombea mwenza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

1 comment

Sikapendi Nakapenda said...

hapa CUF lazima waingizwe mkenge na Wachaga, hawa jamaa wanaitaka hii nchi kwa nguvu yoyote ile, na kwa kuwa wanaona dalili zipo basi hawaoni kama kuna haja sana ya kubanana na waswahili. The day will tell.
Wameshampitisha kushoto Dr. SLAA na wengi watafuata . CHEZEA KANDA YA KASKAZINI WEWE !

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.