BREAKING NEWS : PICHA YA KWANZA KUTOKA MKUTANO MKUU WA CHADEMA MLIMANI CITY, JUA KINACHOJIRI MUDA HUU - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

BREAKING NEWS : PICHA YA KWANZA KUTOKA MKUTANO MKUU WA CHADEMA MLIMANI CITY, JUA KINACHOJIRI MUDA HUU


Hivi sasa Edward Lowassa anaingia ukumbini akiwa akiambatana na John Mnyika, Freeman Mbowe, Salum Mwalimu.
Tayari wamekaa meza kuu na wanasubiri kupewa ratiba. Mshehereshaji anamsifia Lowassa na kuwaambia wajumbe kuwa mabadiliko ni sasa. Wajumbe wanashilia na kusema Rais ni Lowassa 2015 -2020.
Wajumbe wanasimama na kuimba wimbo wa Taifa na baada ya wimbo wa Taifa unaoimbwa na timu ya Movement for Change viongozi wa dini watasimama na kutoa salamu. 
Viongozi wa dini wanaenda jukwaani kwa ajili ya kutoa dua kukabidhi tukio hilo mikononi mwa Mungu kwamaana UKAWA wanaongozwa na Mungu kwa kila jambo.
Salim Mwalimu, anamshukuru Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, kuwa amehakikisha Ofisi ya Katibu Mkuu haikwami kwa lolote katika kutoa mafunzo ya kuwaandaa viongozi kuchukua dola.
Anasema wameimarisha kanda 8 za Tanyanyika kifikra na mtazamo kwa ajili ya kuandaa uchaguzi Mkuu na sasa wanaweza kusimamaia chama katika kila Kata Tanzania na pia anamsifia Mbowe kuwa katika eneo la usajili wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa kuwaingia wanachama wapya waliokuwa nje ya chadema ili chama kipate ushindi.
Salim, anasema usajili uliofanywa na Mbowe wakati wa dakika za mwisho unastahili pongezi kwani wanaenda kushinda kwa kishindo.
Mwisho anasema uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana Chadema walifanikiwa kwa kiwango kikubwa licha ya kuwekewa mapingamizi katika baadhi ya maeneo nchini.
Amewashukuru wale wote waliojitoa kwa ajili ya kukipigania chama ili kiweze kuvuka salama na kushinda katika uchaguzi ujao wa udiwani, Ubunge, nafasi ya Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na nafasi ya Urais.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.