Ahukumiwa miaka 130 jela kwa kumbaka mtoto wa miaka 9 kisha kumuambukiza ugonjwa wa UKIMWI. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ahukumiwa miaka 130 jela kwa kumbaka mtoto wa miaka 9 kisha kumuambukiza ugonjwa wa UKIMWI.

Miaka 130 jela kumuambukiza mtoto UKIMWI Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 UKIMWI. 
Katika kikao hicho Mahakama kuu ya Kenya mjini Kisumu imempata na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limebanwa. 

Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimpata na hatia bwana Okewo kwa kumabaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela. Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu Mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa UKIMWI. Hakimu alimpata na hatia bwana Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe. 

Upande wa mashtaka unasema kuwa bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.


Chanzo: BBC Swahili

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.