ABBAS MAZIKU: MFANYABIASHARA ANAYETAMANI KUFUATA NYAYO ZA BILIONEA MO DEWJI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

ABBAS MAZIKU: MFANYABIASHARA ANAYETAMANI KUFUATA NYAYO ZA BILIONEA MO DEWJI

04.jpgk
Mfanyabiashara wa Kimataifa  Abbas Maziku akiwa katika picha ya pamoja na Mfanyabiashara ambaye pia ni Bilionea kijana Barani Afrika, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji, 'MO'  amabaye anafuata nyayo zake katika kufikia malengo yake kibiashara.
Na Mwandishi Wetu
BIASHARA ya kusafirisha mazao ni miongoni mwa biashara zenye ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na  matajiri wenye asili ya  Kiasia.
Kutokana na sababu hiyo imewafanya waafrika wengi  kuwa na uthubutu katika biashara kwa kuhofia huenda wasifanikiwe na kujitanua kibiashara.
Mbali na ugumu huo lakini pia waafrika wengi hasa watanzania wamejikuta wakiishia  kuwa wafanyabiashara ya kawaida na kupoteza fursa za kimataifa .
Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose fursa ambazo zingeweza kuwafanya wawe na mawazo mengine ya kuchangamkia fursa za kibiashara na kufikiri nje ya boksi.
Makala haya ndani ya mtandao huu yanaangazia mahojiano na mfanyabiashara wa kwanza wa kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha Korosho kwenda nchini  Vietnam  aitwaye Abbas Maziku ambapo alielezea alipoanzia, vikwazo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.

Alipoanzia

Maziku anasema alianza biashara ya kusafirisha mazao mnamo mwaka 2013 baada ya kuvutiwa na mjomba yake ambaye alikuwa na mashamba  yaliyokuwa na  mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao  ambayo Maziku alianza nayo na anaendelea nayo ni pamoja na Korosho, Ufuta, Mbaazi, Choroko, Mtama, Alizeti,  Mashudu yapamba  na pamoja na Pilipili Manga.

Anayapata wapi mazao?

Anasema mazao huyakusanya kutoka kwa wafanyabaishara  wadogo wadogo  ambao hukusanya mazao kwa wakulima pamoja na  minada  inayofanywa na vyama vya ushirika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa kila wiki.

Anayasafirisha kwa njia gani?

Akizungumzia jinsi anavyosafirisha mazao hayo, Maziku anasema hutumia usafiri wa barabara kuyatoa mikoani  hadi kuyafikisha kwenye maghala ambayo hutumia kuyahifadhi kabla ya kufungasha.
"Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa nayafungasha  kwa kutumia vibarua na katika vifungashio vyangu huwa na nembo  inayoonyesha jina la kampuni yangu  na baada ya hapo sampuli hupelekwa katika maabara za kupima kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS  na ndipo hufuatiwa na hatua ya mwisho ya usafirishaji  ambayo huwa natumia Meli za mashirika mbalimbali ikiwemo IPTL, MAERSK  na nyinginezo kwa ajili ya kwenda nchini Vietnam", anasema Maziku.
Anabainisha baada ya hatua zote hizo hufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo watu wa Mamlaka ya mapato T.R.A, wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na Ufugaji, Wanasheria pamoja na maofisa wa usalama wa Taifa ambao uhakikisha hatua zote halali zimefutwa.
Maziku anaweka bayana kwamba  kwa  biashara za kimataifa  taasisi kama  Shirika la viwango TBS na mamlaka ya Chakula na Dawa huwa hawahusiki  bali wahusika wakuu ni SGS.

Anajiendeshaje Kibiashara?

 Maziku anajinasibu kuwa biashara ya mazao  kupeleka nje ya nchi  ni biashara yenye ushindani mkubwa hivyo anakumbuka alianza na mtaji wa sh 2,000,000 na sasa anazungumzia mtaji wa sh mil 200.
 “Si rahisi kufika nilipofikia  kwa sababu biashara hii ina ushindani mkubwa, ninashindana na matajiri wakubwa wenye uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo ingawa nimepiga hatua lakini bado ninahitaji kupanua  biashara yangu zaidi na zaidi”, anasisitiza kwa hisia kali.
 Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara ya  mamilioni ya pesa baada ya ubora wa mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa hivyo ilimpa wakati mgumu ambao aliyumba  kibiashara kutokana na  mtaji wake kukata  hivyo ili mlazimu kuingia benki na kukopa pesa ambazo hadi sasa  bado analipa deni hilo.
 “Nilipata hasara kubwa  sana  ambayo hadi leo hii bado ninalipa  hilo  deni nililokopa benki  ingawa pia fedha kutoka kwenye vyanzo  mbalimbali vya mapato ya biashara zingine ninazozifanya zinaendelea kuifanya biashara hii ya mazao kwenda nje ya nchi iendelee kuwepo” anasema Mfanyabiashara huyo wa kimataifa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.