​Viongozi Vyuo Vya Habari Kukutana Leo Dar es Salaam. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

​Viongozi Vyuo Vya Habari Kukutana Leo Dar es Salaam.

Viongozi wa Serikali za wanafunzi wa vyuo vya habari mkoa wa Dar es salaam wanatarajia kukutana leo saa 7 mchana katika chuo cha Dar es Salaam school of Journalism (DSJ) Kwa lengo la kuzungumzia umuhimu wa kuanzisha umoja wa vyuo vya habari nchini.

Akizungumza nasi muunganishi ambaye pia ni Balozi wa  umoja wa vyuo vya Uandishi wa habari Bw. Michael Charles (Micklove) amesema vyuo vitakavyoshiriki katika mazungumzo  hayo ni Chuo cha /DSJ,PSJ,A3, RAIDA,TSJ, ROYAL na chuo toka Mkoa wa morogoro MSJ, pia vyuo vya Mikoani St. Agustino cha Mwanza,TIA Mbeya, AJTC cha Arusha,St John Dodoma wanataarifa ya kikao cha leo, lengo la kukutana kwa viongozi wa serikali za wanavyuo vya habari nchini ni kuunda umoja utakaotungunisha na kutupa fursa za kushirikiana kimasomo na masuala ya kijamii " alisema Balozi Charles.
Aidha kikao hicho kinafanyika baada ya balozi wa muda Bw. Michael Charles (Micklove) alipopeleka wazo hilo baada kuomba Ushauri wa Kuhitaji kuwepo na Umoja wa  Kuungana  katika wizara ya habari ,vijana na michezo na Utamaduni na kuugwa mkono na Mkurugenzi Msaidizi Ndugu Mh. Raphael Okololo pamoja na vyuo vifuatavyo shiriki wakiwemo viongozi wa juu wa Rais IFM,KAMPALA ,TIA na CBE.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.