Video za wasanii wa Tanzania ndio zimeshika namba 1 kwenye chart za TRACE URBAN na MTV BASE wiki hii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video za wasanii wa Tanzania ndio zimeshika namba 1 kwenye chart za TRACE URBAN na MTV BASE wiki hii

Bet Sasa
Video za wasanii wa Tanzania ndio zimeongoza kwenye chart za vituo viwili vikubwa vya runinga vya kimataifa, MTV Base na Trace Urban wiki hii.
Diamond Trace top10
Baada ya video ya Joh Makini na G-Nako ‘Nusu Nusu’ kukamata nafasi ya 1 kwenye OFFICIAL AFRICAN CHART ya MTV BASE ya Afrika Kusini siku ya Jumanne, video mpya ya Diamond ‘Nana’ aliyomshirikisha Flavour nayo imekamata nafasi ya 1 kwenye chart ya AFRICA 10 ya TRACE URBAN ya Ufaransa Alhamisi wiki hii.
nusu nusu-mtvbase
Diamond aliwashukuru mashabiki wake kupitia Instagram:
“Jus wanna thank all my fans around the world for your major love and Support… I know without you guys this Song wouldn’t been there!!! Also many thanks to @tracenigeria @Trace_inter for keep Supporting Africa Talent…
(Naomba nitumie nafasi hii kuwashkuru Mashabiki na Media zote Kwa support kubwa mnayoendelea kunipa…Bila nyinyi nyimbo hii isingeweza Kufika Hapo…) #Nana #Sankoro NO ONE in AFRICA!!! Click the link on my BIO! to Watch the Video”.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.