Shilole , Mziwanda Warushiana Vijembe Mtandaoni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole , Mziwanda Warushiana Vijembe Mtandaoni

Bet Sasa
Penzi la mastaa wa hapa Bongo, Shilole na Mziwanda linaonekana kupumulia  mashine kwa sasa hivi  baada ya wawili hao kuibuka mtandaoni na kurushiana maneno ya kejeli.
Alianza Shilole kwa kuandika haya;
"Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika'ila sasa kama gari limewaka'aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na maisha yangu'Mimi na yeye baaaaaaasi ...GaNdALaNdiZi"

Baada ya saa 2 Mziwanda alijibu mapigo kwa kuandika;
Mwanaume wa kweli ukaa kimya'sibishani na upumbavu'mwanamke asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa'na kuvumilia mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu'familia na'wasanii wenzangu na wadau'anaanza kunitukana mitandaoni for whaaaat!!! Mxeeeeew'mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu na mtu atakae thamini moyo wangu 'nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari 'mimi nacheka tu
....AsHaNgeDerE

Baadhi wanasema wawili hawa wanasaka kiki huku wengine wakisema huo ndiyo mwisho wa penzi lao.
Tusubiri tuone

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.