Ndikumana wa Irene Uwoya aibukia Stand United, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ndikumana wa Irene Uwoya aibukia Stand United, Ipo Hapa

Mshambuliaji huyo ambaye ni mume wa msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya tayari ameshatua mjini Shinyanga kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho na mabosi wa Stand.
Mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo ambao ndio wanaofanikisha mpango huo waliambia gazeti hili kuwa Ndikumana ambaye alikuwa akichezea soka la kulipwa nchini Ubelgiji atasajili kama mchezaji huru kutokana na kumalizika kwa mkataba wake.
Mshambuliaji huyo ameonyesha nia ya kutaka kucheza soka la kulipwa nchini na ndio hasa kwenye klabu hiyo yenye maskani yake mjini Shinyanga.
“Alikuwapo Mwanza na leo amekwenda Shinyanga kumalizana na mabosi wa Stand na mwenyewe anataka kuwaonyesha kazi ameahidi makubwa kama wakikubaliana kwenye usajili wake anataka kucheza soka kwa mara ya kwanza Tanzania, unajua shemeji yetu huyu,” kilieleza chanzo cha habari.
Shabiki mkubwa wa Stand, Fadhili Mlawa aliliambia gazeti hili kuwa ujio wa Ndikumana kutaziba pengo la Abaslim Chidiebele aliyehamia Coastal Union ya Tanga na timu hiyo ilikuwa inahitaji mchezaji mwenye uzoefu wa kuziba pengo hilo. Chanzo kingine cha habari ndani ya Stand kilisema kuwa timu hiyo kwa sasa inahitaji kuongeza washambuliaji wawili wenye uwezo mkubwa ili kuimarisha safu ya ushambuliaji hivyo ujio wa Ndikumana utakuwa umesaidia.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.