Mtoto Wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown Afariki Dunia...Tazama Hapa Video - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mtoto Wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown Afariki Dunia...Tazama Hapa Video

Bet Sasa
bobi kristina
Imepita miezi sita toka Bobbi Kristina mtoto wa marehemu Whitney Houston akutwe amepoteza fahamu bafuni kwake, na toka kipindi hicho amekuwa kwenye coma kwa muda mrefu hospitalini kabla ya familia yake kumhamishia nyumbani baada ya kuona hakuna matumaini ya ziada.
Familia ya Bobbi Kristina imeweka wazi kuwa mtoto pekee wa marehemu Whitney Houston ameiaga dunia tarehe 27 July 2015 baada ya kipindi kirefu cha kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Taarifa hii imethibitishwa na familia ya Bobbi Kristina huku wengi wao wakiwa na majonzi makubwa kwani hata mazingira aliofia mama yake yanafanana na yale waliomkuta Bobbi Kristina bafuni kwake.
Mipango ya mazishi yake yanaendelea, lakini kwa anaedai kuwa ni mume wa Bobbi Kristina, Nick Gordon huu ndio mwanzo wa upelelezi mzito juu yake kwani anashitakiwa kuwa mtu alietengeneza mazingira ya kumua Bobbi Kristina.
>>> “Sasa hivi tunataka kumzika binti yetu ili ampumzike kwa amani, lakini upelelezi mzito utaanza rasmi baada ya mazishi haya, yoyote yule aliyehusika kumsababishia mwanangu yote haya lazima mkono wa Sheria umpitie”. <<< Bobby Brown.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.