MAYWEATHER "MONEY TEAM " KUPOKONYWA MKANDA WA UBINGWA WA DUNIA. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

MAYWEATHER "MONEY TEAM " KUPOKONYWA MKANDA WA UBINGWA WA DUNIA.

Bondia machachari Floyd "Money" Mayweather Jr alitunukiwa mkanda wa (WBO) wa ubingwa wa dunia katika mchezo wa masumbwi baada ya kumchapa mpinzani wake raia wa Kifilipino, Manny "Pac-Man" Pacquiao mnamo Mei 2, baada ya kumshinda kwa ushindi wa pointi.

Lakini imetangazwa ijumaa ya juzi kuwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 38, atapokonywa mkanda huo kwa kushindwa kutimiza taratibu za umiliki wa mkanda huo.
Ripoti zinasema kuwa Mayweather amekataa kulipa kiasi cha dola laki mbili za kimarekani sawa na zaidi ya milioni 400 za kiTanzania, pili anamili mikanda miwili ya uzito wa kati yaani WBA na WBC ambapo ni kinyume na utaratibu wa umiliki wa mkanda huo wa uzito wa juu wa dunia.Na imeonekana Mayweather hana cha kujitetea kwakuwa amevunja masharti na vigezo vya mkanda wa WBO na hivyo atapatiwa bondia mwingine.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.