Lulu kutoa filamu mpya ‘Ni Noma’ mwishoni mwa mwaka huu, ipo hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu kutoa filamu mpya ‘Ni Noma’ mwishoni mwa mwaka huu, ipo hapa

Bet Sasa
Siku chache zilizopita muigizaji wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael a.k.a Lulu amekuwa aki-tease kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, cover iliyoandikwa ‘Ni Noma, coming soon’ bila kueleza ni kitu gani kinakuja .
Lulu michael
‘Ni Noma’ ni filamu yake mpya na ya kwanza kutoa kwa mwaka huu, ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka alipotoa filamu yake ya mwisho.
“Ni movie yangu mpya, actually ndo itakuwa movie mpya tokea movie ya mwisho ambayo nimeitoa mwaka jana mwezi wa 3, kwahiyo kimekuwa ni kipindi cha mwaka mzima sijafanya movie.” Lulu ameiambia Ayo TV.
Katika filamu hiyo pamoja na Lulu, Staa mwingine ambaye pia amecheza ni Dude. Wengine waliocheza ni waigizaji ambao bado hawajawa na majina makubwa na wengine ni wapya kabisa.
Ni nOma
Lulu amefafanua sababu za kuiita filamu yake ‘Ni Noma’.
“Inaitwa ni Noma, na ina slogan ya Huyu demu ni feki, character yangu ambayo nimeicheza kwenye hiyo movie sio character ya kawaida, so hata jina lake hatukutaka liwe la kawaida. Ni character flani ambayo msichana flani ambaye hajatulia muongo muongo mapepe mapepe, yaani hata sasa katika hiyo movie mara nyingi wanavyomuongelea huyo msichana like wanamuongelea, aah huyo demu noma feki huyo noma, jina tukalipata hivyo kutokana na maneno mengi yaliyokuwa yanaongelewa kwenye hiyo movie na character nzima ya kwangu kwenye hiyo movie.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.