Linah: Tuliwahi kumuomba collabo Wizkid, alitaka milioni 40, ipo hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Linah: Tuliwahi kumuomba collabo Wizkid, alitaka milioni 40, ipo hapa

Muimbaji wa ‘Ole Themba’, Linah Sanga amesema kuwa management yake iliwahi kumtafuta staa wa Nigeria, Wizkid kwaajili ya kumuomba collabo ambayo haikufanikiwa.
linah nostress
Linah ambaye Ijumaa hii anaachia wimbo na video mpya ‘No Stress’ aliyoifanya Afrika Kusini na Godfather, ameiambia Bongo5 kuwa Wizkid aliwatajia kiasi kikubwa cha pesa ambacho hawakuwa wamejiandaa.
“Ni kweli tulimtafutaga sisi Wizkid lakini akawa ametaka hela nyingi, nikasema ngoja kwanza nijipange. Pia alituambia anaweza akatuangalia vile vile kwasababu kwa muda huo alikua busy sana so tujaribu labda next time.”
Linah ambaye kwa sasa yuko chini ya management ya Panamusiq amesema management yake iliyopita ya No Fake Zone-NFK ndio iliyomtafuta Wizkid.
“Alitaka kama shilingi milioni 40 za kibongo, ilikuwa ni muda kidogo. Sisi kwa muda huo tulikua hatuna hiyo hela. Aliongea na one of mtu ambaye aliyekuwa ni meneja wangu.” Alimaliza.
Katika hatua nyingine Linah amesema kuwa tayari amefanya video nyingine na director wa hapa Hanscana, ambayo itakuja kutoka baada ya ‘No Stress’.
Video ya ‘No Stress’ itatambulishwa Ijumaa hii katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.