Hiki ndio kituko ambacho Madam Rita hatokisahau katika Mashindao ya Bongo Star Search. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hiki ndio kituko ambacho Madam Rita hatokisahau katika Mashindao ya Bongo Star Search.

Mashindano ya Bongo Star Search yalionzishwa na Madam Rita yanatarajiwa kuanza hivi karibuni! Mashindano haya yamekuwa na Vituko hasa katika Audition za Mwanzo mwanzo. Madam Ritha kafunguka kuhusu kituko ambacho hatakisahau katika mashindano haya.

Akiongea katika kipindi cha XXL madam Ritha ametaja kitu ambacho hawezi kukisahau katika mashindano haya! Madam Ritha amesema: " Siwezi kusahau jamaa alitokaga huko akiwa ameweka vinyonga kwenye tumbo lake, i will never forget that in my life,ni karibu nizimie, alisimama pale mi nikaona kama, nikamuuliza tumboni umeweka nini, akatoa vinyonga, mimi naogopa sana hivyo vinyonga, amesimama mbele yangu halafu akatia mdomoni, oh my God ilibidi tukatishe Production, niende kupumua kidogo, hiyo sitokaa nisahau, pia kuna mwingine aliacha stage akaja kuniimbia mbele ya uso wangu! dah niliogopa sana, yan ni vituko vingi na tunaona vitu vingi sana.".

Video ya kituko hiki ipo hapa chini au Bonyeza HapaDownload App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.