Batuli Amshukia Kitale Kwa Kuvujisha Picha Hizi Mtandaoni, Zina Siri Gani ? Soma Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Batuli Amshukia Kitale Kwa Kuvujisha Picha Hizi Mtandaoni, Zina Siri Gani ? Soma Hapa

Staa wa mrembo wa Bongo Movie, Batuli ameonyesha kuchukizwa kwake kwa kitendo cha staa mwenzake, Kitale kuvujisha picha hizi  akiwa faragha na mwigizaji chipukizi, Stanbakora ikiwa ni kati ya moja ya kipande cha kazi yao mpya, kwa madai kuwa anaipa ‘promo’.
Kupitia ukurasa wake mtandao Batuli ameeleza kuwa Kitale alimpa picha hizo Mateja ambaye ndiye aliezisambaza kwenye mtandao wa Instagram.
“Kwanza mniwie radhi Watanzania mnachokiona na kinachoelezewa ni vitu viwili tofauti mwenye akili timamu anapata jibu kamili. @mkudesimbaoriginal nikuulize hivi wakati unampa @matejamusa picha ulimwambia ni za nini!? hivi naweza kuwa faragha mbele ya camera!?
Hata kama unapromote movie hii sio kiivyo kama kupromote kitu ndio hivi basi fani yetu imejaa mazumbukuku, hii ni scene iliyopo kwenye movie sioni sababu ya kunichafua kijinga hivi, kizuri kinajiuza @mkudesimbaoriginal  kuandika shit sio njia sahihi ya kupromote kazi yako”- Batuli aliandika.
Je kwako mdau hii imekaaje kwa upande wako ?.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.