A.Y alimpata Godfather kwa ‘kumgoogle’ ..Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

A.Y alimpata Godfather kwa ‘kumgoogle’ ..Ipo Hapa

AY alimtafuta muongozaji maarufu wa video za muziki wa Afrika Kusini, Godfather kwenye mtandao.
11665642_10155977768540413_4151347418411606052_n
Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, AY alisema kilichomsukuma kutaka kufanya video zenye ubora ni wasanii wa Nigeria ambao alihisi ili kwenda nao sawa inabidi kufanya video na waongozaji wanaowatumia.
“Nikasema sasa ili kubanana nao hawa watu inabidi kujua wanafanya kazi na nani na kama wanafanya kazi na huyo mtu iwe tunapishana lugha tu lakini quality tuko nao sawa,” amesema AY.
AY anasema aliamua kutumia internet kujua ni waongozaji gani wanaofanya video za wasanii wa Nigeria.
“Kwahiyo nikaandika pale [kwenye google] ‘Do Me, P-Square directed by’, ikadondoka kwa Godfather sababu video za Godfather zilikuwa zinaandikwa Jude Okoye kaka yao yule mkubwa, haziandikwi Godfather,” ameongeza.
“Kwahiyo nikaangalia pale nikaona ndio huyu, website ya Godfather – ikaja website nikapata website zimeandikwa chini kwasababu kwenye website yake anawekaga production zake, kwahiyo nikampigia.
Anasema baada ya kumpigia Godfather na kujitambulisha, alimweleza kuwa angependa wafanye kazi na wakazungumza bei ambayo walielewana.
Bei waliyokubaliana ilikuwa ni $20,000 ambayo AY aliona ni nyingi kuituma kwake kwa njia ya western union.

Bahati nzuri Godfather alikuwa na safari ya Nairobi alikoenda kufanya matangazo hivyo walikubaliana wakutane huko kulipana na kuzungumza zaidi.
Anasema walikutana Nairobi na kukabidhiana fedha hizo na kupanga tarehe ya kufanya video. Wakati wanakabiadhana, Godfather alimshauri AY waandikishane kwanza japo AY alisema anamuamini na hakukuwa na haja ya kufanya hivyo. Hata hivyo Godfather alimshawishi wakabidhiane kwa kupigwa picha kama ushahidi.
Pamoja na kulipa fedha hiyo yote, ratiba ya Godfather ilikuwa bado imebana kwakuwa P-Square walikuwa wamebook siku 10 za kufanya naye kazi Afrika Kusini. Godfather alimuuliza AY kama anafahamiana na P-Square na kumtaka awapigie kama wanaweza kumpa siku mbili katika siku 10 walizokuwa wamechukua na wao wakakubali.
“Kwahiyo [P-Square] wakatupatia siku mbili nikamchukua mwanangu Marco Chali, nikamuambia Marco hivyo hivyo na passport yako tutanunua nguo huko huko. Ndio hivyo tukafanya Party Zone na ilikuwa ni experience kubwa. Kikubwa zaidi mimi na Marco ndio ilikuwa project yetu ya kwanza.”
-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.