Wema Sepetu Hapendi Unafiki, Kajala Jua Kuwa watu Kama yeye Huwezi Kumalizana Nao Kwenye Simu au Interviews za Radio. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Hapendi Unafiki, Kajala Jua Kuwa watu Kama yeye Huwezi Kumalizana Nao Kwenye Simu au Interviews za Radio.

Ninataman kuona hawa watu wanaelewana tena. Japo upande mmoja unapenda wawe kama walivyo sasa na upande mwingine unatamani zaidi.

Wanapoendelea kujibizana kwenye mitandao na kuongea kwenye media ndio wanazidi kuharibu maana upande mwingine unapata hasira na huenda hali itakua mbaya zaidi!

Naona mashabiki wengi wanazidisha kuchochea mambo, muwaache watakuja kupatana na mtaongea nini wakati huo? Kwa taarifa za uhakika sio khs mwanaume ni mambo ambayo hata hivyo yanaweza kusawazishwa!! @new_kajala unamjua Wema vizuri sana kuliko hata sisi, unajua madhaifu yake na nguvu zake kama una nia ya kweli malizana nae iwe kwa amani au shari sio kila siku story ni ile ile.... ungemfuata Wema uhakikishe kama kweli hawezi kukusamehe!

Kuna kitu khs Wema hapendi unafki au hakai na kitu moyoni, aina ya watu kama yeye huwezi kumalizana nao kwenye simu au interviews....Wema ana huruma sana ukionana nae ana kwa ana mkazungumza ni mwepesi kuachilia, kuna nguvu ya upendo iko ndani yake ndo husababisha hasira kusikia upande wako....ukimpenda mtu sana si unajua inakuwaje akikuudhi?
Basi Wema upendo wake kwa Kajala sio fake ndo maana linapokuja suala la Kajala huonesha hisia zake za wazi...na upendo wa namna hii wakisuluhisha...bado kuna nafasi ya kuwaona tena pamoja kama kweli walipendana kwa dhati.

So haters....habari ndo hiyo, watapatana !!

By Mrekebishatabia

UNAWEZA KUJISHINDIA SIMU AINA YA HUAWEI MATE 7 NI RAHISI SANA BONYEZA HAPA KISHA BOFYA "VOTE" ALAFU FUATA MAELEKEZO.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.