VIATU VIREFU VYAMUUMBUA KIM KARDASHIAN - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

VIATU VIREFU VYAMUUMBUA KIM KARDASHIAN

Staa hot, modo wa ukweli, Kim Kardashian.
STAA hot, modo wa ukweli, Kim Kardashian, almanusura aanguke kufuatia kiatu alichokivaa kuwa kirefu, hivyo kusababisha ajikwae, Ijumaa iliyopita huko Beverly Hills.
Kim alikwenda kufanya shopping kwenye Duka la Celine on Rodeo Drive lililopo Beverly Hills ambalo huuza mavazi ya kike, ndipo akakutwa na masaibu hayo ya kuteguka na kutaka kuanguka lakini aliweza kuhimili.
Mrembo huyo ambaye ni mtangazaji wa Kipindi cha Keeping up With the Kardashians, ni mke halali wa rapa Kanye West, sasa hivi ana mimba ya mtoto wa pili baada ya North West.
Wakati akienda kujadiliana bei na muuzaji, Kim alisikika akisema: “Ooh Mungu wangu, natamani kuvitoa hivi viatu. Havinipi uhuru. Sitaki kuvivaa, nataka kuondoka ili nikavitoe.”
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.