Vanessa Mdee ana video ya wimbo mpya tayari ‘can't wait for you to see it’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vanessa Mdee ana video ya wimbo mpya tayari ‘can't wait for you to see it’

Vanessa Mdee anaendelea kushambulia kwa kasi na haoneshi dalili za kupumzika.
11275390_875691035830033_616185966_n
Akiwa anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake ‘Nobody But Me’ aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O, Vee Money amesema tayari mkononi ana video ya wimbo mpya.
Vanessa ametoa tangazo hilo kupitia #BaseTwitterView ya MTV Base ambapo mashabiki walikuwa wakimuuliza maswali kwenye mtandao wa Twitter.
“Just got the first cut of my new video, can’t wait for you to see it ,” alijibu swali la Clerment @_MC_Sfoj aliyeuliza, “what are you currently working on music wise?”
Katika hatua nyingine Vanessa anayewania tuzo za MTV MAMA mwaka huu, anatarajia kwenda kutumbuiza jijini Lagos.
“Yaaaas I’m coming out to Lagos to perform for the 3rd time in 2 weeks,” alijibu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !