Shamsa Ford Aonyesha Jeuri Kumlea Mtoto Wake Bila Msaada wa Baba Yake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford Aonyesha Jeuri Kumlea Mtoto Wake Bila Msaada wa Baba Yake.

Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana.
Amesema tangu wamwagane na mzazi mwenzake, mtoto wake hajawahi kumuuliza baba yuko wapi kitendo kinachomfanya azidishe mapenzi kwake kwani hata yeye alilelewa na mama yake bila baba.
  • “Kama baba yake alikuwa akinipiga mbele yake au kuja akiwa amelewa tilalila unafikiri mtoto atamkumbuka? 
  •   
  • Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.