SHAMSA AWAKANDIA MABWANA ZAKE, KISA NINI ? IPO HAPA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SHAMSA AWAKANDIA MABWANA ZAKE, KISA NINI ? IPO HAPA

Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kuwakandia mabwana aliowahi kutoka nao kimapenzi na kusema kuwa ni wababaishaji na sasa ni bora atafute mwanaume wa kumuoa.
Akipiga stori na Amani, Shamsa anayetikisa na Filamu ya Chausiku alisema, kwa sasa amejipanga kuolewa wakati wowote iwapo tu mwanaume mwenye sifa anazozitaka atajitokeza.
“Wengi niliowahi kuwa nao ni wababaishaji tu na wala sikuona mwanaume wa kuweza kunioa. Kwa sasa nimeshakua mtu mzima na ikitokea wa kunioa nipo tayari,” alisema Shamsa.
Awali Shamsa alikuwa akitoka na mtu aliyetambulika kama Dick na kupata naye mtoto mmoja, baada ya hapo ilidaiwa bidada huyo kaingia kwenye uhusiano na Nay wa Mitego.
-gpl

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.