Hii Ndio Top 10 Ya Nchi Tajiri Afrika , Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hii Ndio Top 10 Ya Nchi Tajiri Afrika , Ipo Hapa

AfricaUkisema uingie mtaani sasa hivi kumuuliza mtu mmojammoja ni nchi ipi tajiri zaidi Afrika huenda ukapata majibu tofauti lakini uhakika wa hilo upo kwenye ripoti mpya iliyofanywa kwa bara la Afrika.
Nigeria ni nchi ambayo Dunia inajua kuhusu mafuta yao, inajulikana pia majina ya matajiri wao kama akina Alhaji Aliko Dangote.. mengine yanayosikika sana kutoka huko ni ishu kama za mashambulio ya Kigaidi, leo imeingia kwenye headlines nyingine.
Utafiti uliofanyika umekuja na majibu tayari, Nigeria ndio nchi inayoongoza kwa utajiri sasahivi ndani ya Afrika… South Africa iko nafasi ya pili alafu zinafuatia nchi nyingine.
Ninayo list ya Top 10 ya nchi zote hapa.
No.1: Nigeria, hii ina sifa nyingine kubwa kuwa nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi Afrika, na pia utajiri wake unatokana sana na uzalishaji wa mafuta.
No.2: South Africa, sehemu kubwa ya Utajiri wao inatokana na uchimbaji wa madini.
No.3: Misri
No.4: Algeria, nao wako kwenye list ya wauzaji wakubwa wa mafuta na gesi.
No.5: Morocco, uwekezaji wao mkubwa uko kwenye Utalii, viwanda vya nguo na Kilimo.
No.6: Sudan.. sio rahisi kukutana na nguo imeandikwa ‘Made in Sudan’, lakini wao ni wauzaji wakubwa sana wa pamba duniani.
No.7: Kenya, biashara yao kubwa ni chai na kahawa.. sikuwahi kujua kumbe hata biashara ya kuuza maua kwenda Ulaya nayo ni biashara inayoingiza pesa nyingi Kenya.
No.8: Angola.. japo walipitia kipindi kigumu cha vita kwa zaidi ya miaka 25, bado madini, mafuta na kilimo vimeiweka nchi hiyo ndani ya Top 10 ya nchi tajiri Afrika.
No.9: Libya.. Hii ndio nchi ya kwanza Afrika ambayo wataalam wamesema kuwa ina akiba kubwa ya mafuta ndani ya Afrika mpaka sasa, na hiyo ndio inayoiingizia nchi hiyo pesa nyingi zaidi kila siku.
No.10: Tunisia.. wao biashara yao kubwa ni spare za magari, kuuza mafuta na utalii.
-millardayo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.