AUNT, MKE WA IYOBO PACHIMBIKA ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

AUNT, MKE WA IYOBO PACHIMBIKA !

STAA mkali katika anga la filamu Bongo, Aunt Ezekiel, ameingia katika malumbano makali kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na mzazi mwenzie, Moses Iyobo, Mwengi mpaka kufikia hatua ya kuwaita watoto zao majina yasiofaa.
Chanzo makini kabisa kinadai kuwa hapo awali kabla ya Aunt kujifungua, Mwengi alitoa tamko kuwa kama staa huyo angejifungua basi atajifungua chura, kitu ambacho kilimkera sana na kuahidi kuwa atafungua mdomo wake atakapozaa.
10375826_637562372992918_14808219_nStaa mkali katika anga la filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Baada ya kusikia madai hayo Amani lilimtafuta Aunt, ambapo alisema kuwa aliamua kusema hivyo kutokana na mtoto wake kuitwa chura.
“ Hivi wewe mtu akuitie mtoto wako chura kweli ungejisikiaje basi nami nikasema kama wangu chura wa kwake panya ili kila mtu auguliwe,” alisema Aunt.
IYOBO67Kwa upande wa Mwengi, alisema;
“ Siwezi kumuita mtoto wa mwanamke mwenzangu hivyo hata siku moja kama kuna sehemu aliona nimeandika hivyo anioneshe maana mimi kwa sasa niko bize na mambo yangu.”
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !