Zari The Boss Lady " Watanzania Wamenikubali Kama Mtu Wao, Ntahamishia Makazi na Biashara zangu Hapa" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zari The Boss Lady " Watanzania Wamenikubali Kama Mtu Wao, Ntahamishia Makazi na Biashara zangu Hapa"

Zari Tlale aka The Bosslady amesema upendo anaoupata baada ya kuanzisha uhusiano na Diamond Platnumz, umemfanya agundue kuwa watanzania wamemkubali kama mtu wao.Akiongea na Clouds FM/TV asubuhi hii,

Zari amesema tangu ameanza kuja Tanzania amekuwa akipokea upendo zaidi kutoka kwa watanzania kiasi ambacho kimemfanya ajisikie kama yupo kwao. “Siwezi hata kulalamika, watu wa Tanzania ni wakarimu sana ni watu wazuri sana, kwangu mimi sijapata hata tatizo, siwezi hata kusema kitu chochote kibaya kuhusu watu wa Tanzania,” alisema. “Wamenikaribisha kama ni mtu wao na sasa mimi ni wao hivyo ni yote ni heri kabisa,” aliongeza. Katika hatua nyingine Zari amesema Tanzania itageuka kuwa makazi yake ya mara kwa mara na mipango iliyopo ni kuanzisha mradi wa kibiashara nchini lakini baada ya kufanya utafiti na kubaini fursa za uhakika.

“Siwezi tu nikafungua biashara hapa eti kwasababu mimi ni maarufu nikafungua tu biashara ya kijinga na nikidhani ninaweza nikauza wazo langu la kijinga kwa watu hapa, wao sio wajinga wanatumia hela zao hivyo nahitaji kubaini wapi kuna hitaji, kipi naweza kufanya na hapo ndipo ntaenda na kuwekeza fedha zangu.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.