Utata Mpya Mkubwa Waibuka Mshindi wa Pambano la Ngumi Kati ya Mayweather na Manny Pacquiao, Karatasi za Matokeo zaonyesha Manny Pac Ndio Mshindi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Utata Mpya Mkubwa Waibuka Mshindi wa Pambano la Ngumi Kati ya Mayweather na Manny Pacquiao, Karatasi za Matokeo zaonyesha Manny Pac Ndio Mshindi

Bet Sasa
UTATA umeibuka kutoka Pambano la Karne baina ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililofanyika juzi ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani.

Karatasi ya kuandika matokeo raundi kwa raundi ya majaji wote watatu, Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti inaonyesha bondia aliyekuwa kona nyekundu, Pacquiao ndiye aliyeshinda pambano, wakati mtangazaji 'MC' wa pambano akamtangaza bondia wa kona ya bluu, Mayweather ndiye mshindi.

Inaonekana kama majaji walijichanganya katika kutumia karatasi hizo na pointi za Mmarekani, Mayweather 'Mtu Pesa' wakizihamishia kwa Mfilipino, Pacquiao, lakini kwa nini iwe kwa majaji wote watatu?

Hii inazidi kuzua shaka kwamba inawezekana Mayweather alipewa ushindi kimakosa bali kwa mujibu wa karatasi za majaji mshindi ni Pac Man aliyekuwa anatokea kona nyekundu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.