Shilole Aapa Kutopiga Picha Za Faragha Akiwa na Mpenzi Wake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole Aapa Kutopiga Picha Za Faragha Akiwa na Mpenzi Wake.

Bet Sasa
Staa wa Bongo movies na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesema kuwa  hatapiga tena picha akiwa faragha na mchumba wake Nuh Mziwanda kwani zimekuwa zikivuja bila yeye kujua na kusababisha adhaulike kwenye jamii.
Shilole Aapa Kutopiga Picha Za Faragha Akiwa na Mpenzi Wake
Akizungumza na gazeti la Tanuru la Filamu, Shilole alisema alikuwa akifanya hivyo ili badaye  akiwa yuko mbali na mpenzi wake apate kuangalia jinsi walivyokuwa wakifurahishana lakini mambo hubadilika zikivuja na hivyo kuwa kwaza mashabiki wake ambao wanaheshimu sanaa yake
 “Naapa kutopiga picha za utupu nikiwa faraga na mpenzi wangu kwani awali nilikuwa nikifanya hivyo pasipo kujua kama zinaweza kuvuja kwenye mitandao ya kijamii kwani mpaka sasa sijui huwa zina vujaje na ili kukomesha hali hiyo sitafanya upuuzi huo tena” alisema Shilole.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.