Salman Khan Wa BollyWood Ahukumiwa Jela Miaka 5 Kwa Mauaji !! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Salman Khan Wa BollyWood Ahukumiwa Jela Miaka 5 Kwa Mauaji !!

Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan.
Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa mjini Mumbai.
Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002.
Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Jaji wa mahakama hiyo, Khan anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
-BBC

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.